Angalia! Usiwe gugu!

Heeeeeee! This post.... I don't know what language to use for emphasis. I will choose swahili.
Katika maisha binadamu tunatabia moja ya kuiga vitu. Yani, hasa hapa Tanzania ninapotoka mimi, maadamu siwezi ongelea inchi nyingine kwa maana sijawahi fika.
Hii tabia ya kuiga imeingia kwenye shughuli muhimu kama biashara. Na nimekutana na watu wengi sana wanaolalamika kwamba anaanzisha biashara na watu wengi huiga.
Juzi nimepita pale stendi ya mabasi ya makumbusho, na kusema kweli nilipigwa na butwaa. Sikutegemea kukuta wauzaji wa bisibisi (popcorn) wakiwa wengi hivyo na tena kujipanga kwenye mistari kadhaa. Kwakweli sikufurahia lakini sikuweza kijizuia, nilicheka moyoni. Nilijisemea, sijui nani gugu au nani ni ngano (mtalamu hasaa).
Sasa basi, naomba niongee na wewe ambae unaiga.
Je umewahi kujiuliza maswali haya?
1. Kwanini ninaishi au kwanini niliumbwa?
2. Je niliumbwa niige?
3. Je ninachokiiga ninakipenda kukifanya?
4. Je siwezi fikiria wazo jipya?
5. Je hili swala litanisaidia kutimiza malengo yangu maishani?
6. Je mkakati wangu wa baadae kuhusu hii biashara ninayoiga ni upi?
7. Je ninavyo iga ninaweza kuwa bora kuliko yule ninaye muiga?

Kuiga sio kitu kigeni, ila jua madhumuni ya kuiga na pia kuwa tayari kuwa bora kuliko unayemuiga ili wewe uwe ngano na yeye awe gugu. Na zaidi ya yote jua katika maisha, lazima magugu yafe kifo kibaya.

Ukiweza jibu maswali haya machache, uamue kama utapenda kuwa mtu aliye na mawazo yake halisia au utapenda kuendelea kuiga vya watu.

Je mawazo halisia yanatoka wapi?
1. Kusoma vitabu vyenye tija maishani, vitabu vya kukuongezea upeo.
2. Kukaa na watu na marafiki wenye mawazo chanya na endelevu.
3. Kujijua wewe ni nani, na kwanini uliumbwa na Mungu.
4. Kujiwekea malengo maishani.
5. Kujenga tabia ya kutafakari mambo endelevu kwa undani zaidi.

Na kama umependa biashara fulani, na ungependa kuifanya/kuiga. Basi kubali kuwa mwanafunzi wa biashara hiyo.
1. Jua biashara hiyo inaingizaje kipato.
2. Jua kiasi gani unapaswa uekeze ili upate kipato toshelevu.
3. Jua ni jinsi gani unaweza kuikuza biashara yako mpaka iwe ya kimataifa.
4. Jua ni nini changamoto za biashara na jinsi ya kuzishinda.
5. Jua faida kuu za baishara hiyo.
6. Jiulize, Je tukiwa wengi tunaofanya biashara hii, nitakuwaje kinara zaidi ya wengine. (In other words, know your competition and how to beat your competition ~ Kwamaneno mengine jua washindani wako na jinsi ya kuwashinda)

Biashara kusema kweli ni ushindani. Kataa ama kubali. Utashindana kwanza na wewe mwenyewe ili uweze kuwa bora zaidi ya jana yako. Na pili utashindana na watu wengine wanaofanya biashara sawa na yako ama inayofanana kidogo na yako.

Sasa basi kabla ujaamua kuiga ama kuendelea kuiga, jijibu maswali hayo hapo juu na mengine yaingiayo moyoni mwako kutokana na maswali hayo. Na kisha chukua hatua ya kuandika hiyo biashara katika daftari, andika majibu yote na makusudi na malengo yako yote juu ya hiyo biashara.  Chukua hatua ya ziada na kuandika njia utakazo tumia kufikasha malengo ya biashara yako.
Na siku zote kumbuka kwa lolote uamualo kufanya usikubali kushindwa, kama jambo linawezekana.

Mpaka majaliwa.

Comments

Popular Posts